Inatupasa kuzaliwa mara ya pili kwa maji na Roho
Mungu(God), hapo mwanzo alipoumba mbingu na nchi, Yeye pia aliumba ulimwengu wa milele, mbingu na jehanamu. Yeye pia aliumba mwanadamu kwa mfano Wake Mwenyewe. Hata hivyo, kwa kuwa mwanadamu wa kwanza, Adamu, alitenda dhambi mbele za Mungu(God), watu wote imewapasa kufa mara moja. “Na kama vile watu wanavyowekewa kufa mara moja, na baada ya kufa hukumu” (Waebrania 9:27).
Kifo cha miili yetu ndiyo njia ya kupita kwenda kwenye uzima wa milele. Wale wasio na dhambi wataingia katika ulimwengu wa milele wa mbingu na kufurahia milele furaha ya kuwa mtoto wa Mungu(God), ilhali wenye dhambi watatupwa katika “ziwa la moto na kiberiti” (Ufunuo 20:10) na watateswa mchana na usiku milele na milele.
https://www.bjnewlife.org/
https://youtube.com/@TheNewLifeMission
https://www.facebook.com/shin.john.35
Tulizaliwa duniani humu, lakini kabla ya hapo Mungu(God) alikuwa tayari anatujua. Alijua kwamba tungezalika tukiwa wenye dhambi na akatuokoa sisi sote waumini kupitia ubatizo...
Kwanza, ningependa kufafanua dhambi ni nini. Kuna dhambi zilizofafanuliwa na Mungu(God), na kuna dhambi zilizofafanuliwa na wanadamu. Neno dhambi, kwa Kigiriki, lina maana ya...
Swali 1: Nimekuwa nikisoma vitabu ambavyo ulinitumia kwa fadhili na nimeona baadhi ya dhana zako kuhusu ubatizo wa Yesu zinavutia. Je, unaweza kuniambia kile...